Chunya,
Mbeya
Waziri
wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ametoa wito kwa wakulima nchini kuwa na
Vitambulisho ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za mkulima kwa urahisi kama
vile aina ya kilimo anachofanya, eneo analotoka, mazao anayolima na taarifa
nyingine muhimu za utambulisho wake.
 |
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa masoko ya minada ya Tumbaku wa mwaka 2020/21
uliofanyika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 26,
2020 |
Waziri
Hasunga aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa masoko ya minada ya
Tumbaku wa mwaka 2020/21 uliofanyika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya mwishoni mwa
wiki iliyopita Juni 26, 2020. Akifungua masoko hayo Waziri alisisitiza kuwa ni
muhimu wakulima kuwa na vitambulisho kwani kilimo ni moja ya Sekta muhimu za
uchumi wa Taifa letu kutokana na kilimo kuchangia pato la Taifa pamoja na asilimia 30 ya fedha za kigeni kwa mahitaji ya
kibiashara, ajira, chakula, na malighafi za viwandani.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa masoko ya minada ya Tumbaku wa mwaka 2020/21 uliofanyika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 26, 2020 |
Katika
hotuba ya ufunguzi huo, Waziri alitoa maelekezo kwa maafisa Ugani wafanye kazi
zao kwa bidii wakizingatia kuwahudumia wakulima mashambani. Aliongeza kuwa
maafisa ugani watumie muda wao mwingi mashambani ambapo ndipo wanapohitajika
kutumia taaluma zao kuongeza uzalishaji wa kilimo chenye tija nchini.
“Kila
mkulima asajiliwe, ajulikane yuko wapi analima kiasi gani, analima zao gani,
analima ukubwa gani wa shamba, kiwango cha mavuno anachopata pamoja na
changamoto alizonazo,” alisisitiza Waziri
Aidha,
ameitaka Bodi ya Tumbaku nchini kuongeza kasi ya utafutaji wa masoko ya tumbaku
inayozalishwa nchini kutokana na changamoto ya kupungua kwa wanunuzi wa zao la
tumbaku pamoja na bei ya zao hilo kuendelea kushuka hivi karibuni. Jambo ambalo
linasababisha kipato kwa wakulima kuathirika na mapato ya Serikali kupungua.
 |
Mnada wa Tumbaku kwenye ghala la Chama cha msingi Lupa AMCOS
|
Pamoja
na mambo mengine ameagiza Viwanda vya tumbaku visiuzwe bali vifufuliwe ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuendeleza na kuimarisha Uchumi wa
viwanda, ambapo viwanda hivyo vitatumia mazao na malighafi za kilimo, kuongeza
ajira na kukuza Sekta ya Viwanda.
Mrajis
wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akizungumza katika uzinduzi huo
amesisitiza Vyama vya Ushirika kuendelea kujikita katika kujenga na kuimarisha
mitaji yake ya ndani ili kuwa na nguvu zaidi za kiuchumi katika Vyama
itakayowezesha kukopesheka vizuri kwa riba nafuu kutoka kwenye taasisi za
Kifedha na mabenki.
Dkt.
Ndiege alieleza kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na Serikali
itaendelea kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaobainika kufanya shughuli za
ushirika katika vyama bila kufuata taratibu au watumishi watakaokiuka maadili
ya utumishi wa Umma, akimalizia kwa kuwaomba wadau kuendelea kutoa ushirikiano.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Tumbaku (T.C.J.E), Bw. Emmanuel
Charahani katika maelezo yake amesema
kuwa baadhi ya changamoto katika kilimo hicho ni kuendelea kuporomoka kwa bei ya Tumbaku. Akifafanua kuwa msimu wa 2016/17 wastani wa
bei ulikuwa Dola 2.06 lakini msimu huu ambao soko la Tumbaku limefunguliwa bei
ya wastani ni Dola 1.60. Hali inayopelekea wanunuzi na wakulima wa Tumbaku
kuzidi kupungua na kuiomba Serikali kusaidia kunusuru hali hiyo kwa kutafuta
wanunuzi zaidi wa Tumbaku.
Charahani
amesema matarajio ya kitaifa ni kuzalisha kilo millioni 57 za tumbaku ambazo
zinauzwa sasa, hii ikiwa imetokana na hali ya hewa mwaka huu ya mvua nyingi
zilizosababisha mbolea kupotea ardhini.
Aidha,
Mwenyekiti Charahani ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jinsi
inavyoendesha na kusimamia shughuli mbambali za kilimo kwa kutetea maslahi ya
watu wanyonge. Ameipongeza pia Serikali kwa kuondoa baadhi ya tozo na kodi za Tumbaku
ambazo zitasaidia kujenga hoja zenye nguvu katika kujadiliana bei ya Tumbaku na
Wanunuzi.