|
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akitoa maelekezo kwa viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo vya Bariadi Teachers SACCOS, ATAPE SACCOS,Bariadi Hospital SACCOS na Roots and Shoots SACCOS
|
Mrajis
wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege amewataka Maafisa Ushirika nchini kuongeza
nguvu ya usimamizi katika Vyama vya Ushirika kwa kuweka mpango wa kuvitembelea
Vyama hivyo mara kwa mara na kuangalia shughuli zinazofanyika.
Dkt.
Ndiege ametoa maelekezo hayo jana Juni 09, 2020 katika Kikao cha pamoja na
Maafisa Ushirika wa Wilaya za Bariadi Mji, Bariadi Vijijini na Itilima alichokifanya
akiwa kwenye ziara ya siku moja mkoani Simiyu.
“Ni
muhimu kuweka usimamizi imara ili kuondoa dhana ya kufanya uchunguzi, ni bora
kugundua tatizo kabla halijatokea na kulidhibiti kuliko kusubiri litokee na
kuanza kuchukua hatua,” amesema Mrajis wa Vyama vya Ushirika.
Aidha,
Dkt. Ndiege amewataka Maafisa Ushirika kufuatilia makusanyo ya Mfuko wa
Usimamizi na Ukaguzi kutoka Vyama vya Ushirika ili kupata fedha za kusimamia
Vyama hivyo, na amesema kuwa fedha za makusanyo hayo zitaendelea kupelekwa
mikoani na wilayani ili kuongeza usimamizi na kuimarisha Ushirika nchini.
Akizungumzia
Mfumo wa Ushirika katika Ununuzi wa mazao mchanganyiko, Dkt. Ndiege amesema
mfumo huo haujafanya vizuri katika baadhi ya mikoa kwa kuwa mfumo ulianza katikati
ya msimu ambako tayari kulikuwa na mfumo huria katika unuzi wa mazao.
“Kwa
sasa Serikali imeshaelekeza mazao mchanganyiko kuuzwa kupitia Vyama vya
Ushirika ni muhimu tukajipanga kwa kuwaelimisha wakulima umuhimu na faida ya
kuuzia mazao yao kupitia ushirika chini ya mfumo wa Stakabadhi ya Soko Ghalani,”
amesema Dkt. Ndiege.
Katika
kikao hicho Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Ibrahim
Kadudu kupitia taarifa ya Ushirika ya Mkoa alisema Vyama vya Ushirika vya pamba
Mkoani humo vinakabiliwa na changamoto ya malipo ya Ushuru kiasi cha Shilingi
bilioni 3.9 na bado wakulima zaidi ya 11,047 wanadai fedha zao za pamba kiasi
cha Shilingi bilioni 3.4 kwa msimu uliopita.
|
Mrajis Msaidizi Mkoa wa Simiyu Ibrahim Kadudu akiwasilisha Taarifa ya Ushirika Mkoa wa Simiyu kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege |
Katika
ziara hiyo ya siku moja mkoani Simiyu, Dkt. Ndiege alikutana pia na viongozi wa
Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU 2018) na kuwataka kuhakikisha
muafaka wa mgawanyo wa mali kati ya SIMCU na SHIRECU unafanyika haraka ili
kuruhusu uwekazaji katika mali hizo ambazo ni viwanda vya kuchakata pamba
vilivyopo Lugulu, Sola na Malampaka.
|
Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiegwe (wanne kushoto) akiwa pamoja na Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Simiyu, Ibrahim Kadudu na Wajumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu
|
“Viwanda
hivi vinapaswa kufufuliwa ili vifanye kazi na haviwezi kufufuliwa mpaka mmiliki
afahamike; hivyo, ni lazima kuwepo na maridhiano ya mgawanyo wa mali na madeni
kati ya SIMCU na SHIRECU,” alisema Mrajis.
Mwenyekiti
wa Bodi wa SIMCU, Emanuel Mwerere alisema kuwa makubaliano hayo yanachelewa
kwasababu wanachama wa SIMCU waliamua kupitia Mkutano Mkuu kuwa wapo tayari
kupokea mali kutoka SHIRECU lakini hawapo tayari kupokea madeni kutoka SHIRECU kwa
kuwa viwanda hivyo vimebaki magofu hivyo watapata gharama mara mbili ya kufufua
na kulipa madeni hayo.
Aidha,
Dkt. Ndiege vilevile alikutana na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na
Mikopo (SACCOS) vya Bariadi Teachers SACCOS, Simiyu ATAPE SACCOS, Bariadi Afya
SACCOS na Roots and Shoots, ambapo alitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya changamoto
zinazojitokeza katika usimamizi na uhamasishaji wa maendeleo ya ushirika
nchini.
|
Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Fedha vya Bariadi Teachers SACCOS, ATAPE SACCOS, Bariadi Hospital SACCOS na Roots and Shoots SACCOS |